Dogo Janja ni msanii wa bongofleva ambaye mwenye Smash hit
iitwayo My Life ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika vituo mbalimbali.
.
Staa huyo kayaongea haya>>>>Prezzo
alitaka kufanya remix ya My Life lazima haikuwezekana kwasababu Radio
and Weasel walikuwa wamefanya kwahiyo My Life ni wimbo ulionifungulia
mipaka kuna collabo nyingine zinakuja’– Dogo Janja
‘Radio
and Weasel wao ndio walitokea kuipenda ile single yangu ya My Life basi
wakafanya mawasiliano na Babu Tale wakakubaliana, kwa ambavyo
ilivyokuwa pia kwa upande wangu ikashindikana kufanya remix ya hiyo
single kwahiyo nilikuwa nimewapanga Maua Sama na G Nako‘- Dogo Janja
‘Kwahiyo kutokana na Prezzo
kukosa nafasi ya kuifanya remix ya wimbo wangu wa My Life basi
tukakubaliana kuwa atanishirikisha kwenye wimbo wake mpya ambao muda
wowote nitaenda Kenya kwaajili ya kushoot video’- Dogo Janja
Source. Millardayo.com
EmoticonEmoticon